YALIYOMO
SHUKRANI
Shukrani
za dhati kwa Mungu baba aliye juu kwa kunipa uhai na kuniwezesha kufanikisha
kutoka kwa kitabu hiki ingawa ilikuwa kazi ngumu bila msaada wako Mungu
nisingeweza kufanikisha hili.
Pia
shukrani zangu ziwafikie familia yangu na marafiki zangu kwa kunipa ushirikiano
wa kutosha Mungu awabariki nyote.
Bila
kukusahau wewe uliyechukuwa muda wako kosa kitabu hiki Mungu akubariki sana na
kukutia nguvu katika maangaiko yako ya kila siku.PAMOJA TUNAWEZA.
KILELE CHA UBEPARI NA TISHIO LA USHOGA AFRIKA
Kitabu hiki kinaelezea
maisha halisi ya mwananchi wa hali ya chini katika bara la Afrika,ususani chini
ya ya jangwa la sahara.
Harakati
zao za kujinasua katika umasikini uliokisiri?
Ni kwa nini umasikini unazidi kuongezeka ndani ya
bara letu lenye kila aina ya rasilimali?.Je ni kwa nini wanasiasa wamekuwa
vigeugeu?.
Nani anayeanzisha
maandamano ya ukombozi katika nchi nyingi za Africa?
·
lengo la kuleta ushoga Africa nini?
·
ni nani wa kulaumiwa katika hili?
Kitabu hichi
kimechambua kwa undani nini cha kufanya ili kujikomboa katika hili janga
lilokumba bara letu la africa.
hapa tulipo sasa ni KILELE
CHA UBEPARI KATIKA BARA LETU.(KILELE CHA UBINAFSI WA MALI)
UTANGULIZI
Tujikumbushe kwanza
Africa ilitoka wapi ?Africa kama mabara mengine dunia lilikuwa bara lenye wananchi wanaojiongoza
kwa mila na desturi za makabila yao.Hii
ikimaanisha kuwa sheria na taaratibu za kuishi zilizingatia sana mila na
desturi hiyo basi kila ukoo ulifanya kila mbinu ili uweze kukubalika katika
kabila husika na waweze kupewa uongozi wa kabila husika,hali hii ilifanya kupatikana
kwa ukoo zenye nguvu ya kutawala na kutoa maamuzi mazito kuhusu makabila
husika.
Katika hali hii iliongeza ubunifu hasa katika
maeneo ya uzalishaji wa mazao na vifaa vya kivita na mafunzo ya kijeshi.hii
ilisaidia sana ukuwaji wa maeneo na kusababisha koo na makabila mengine madogo
madogo kufa kwa sababu ya kushindwa kivita
na mali zao walizokuwa wakimiliki kupokonywa na makabila hayo yakageuka
vibaraka wa makabila yale makubwa.
Makabila mengi
yalipotea nakutofahamika tena kwenye uso wa dunia kutokana na sababu hizo na
mengine yaliweka makazi kwenye maeneo yenye wanyama wakali ,mafuriko na wadudu
waambukizao maradhi na wakashambuliwa na
magonjwa,wanyama wakali na mafuriko na
kuisha taratibu baada ya kuanza kutawanyika kukimbia majanga hayo.
Je
ubepari ulianzia wapi?
Tutambue kuwa ubepari
huanza kwa hatua hiyo basi historia inaonyesha kuwa toka aumbwe Adamu na Eva
hapo ndipo ubepari ulipoaza ukiwa na sura ya ubinafsi(maana ubinafsi ni mtoto
wa ubepari).Adamu na Eva walipewa dunia waitawale na wafaidi kila kitu
kilichopo ndani ya dunia hii mto,maziwa ,asali ,matunda, majani na kadhalika.
Adamu na Eva alijua
kabisa bosi wao ni Mungu aliye juu mmiliki wa mali zote walizokabiziwa
wazitumie mpaka pumzi yao pia ilikuwa ni mali yake.
Adamu na Eva walingizwa kishawishini na shetani wamsaliti
Mungu na kubinafsisha mali zake zote walizokabiziwa na wazimiliki wao kwa
ushirikiano na shetani mkuu wa kuzinu.
Kutokana na hilo bwana
Mungu alichukiza na ile hali na kuamua kuwatupa nje ya ile bustani ya edeni na
kuwaacha wakahajitafutie wenyewe chakula na mahitaji yao ya kila siku.
Katika hali hii basi
tutaona kuwa mwenyekiti wa ubepari duniani ni SHETANI.
Maana ndiye muanzilishi
waubepari duniani toka enzi za Adamu na Eva ni yeye aliyewapa ujasiri wakina
Adamu na Eva waukubali ubinafsi na kuachana na mpango wa Mungu ulikuwa unaweka
umoja wa kila kitu.
Je
dhumuni la ubepari ni nini?
Katika hali ya kawaida
tunaona kuwa dhumuni kubwa la ubepari
dunia ni uuwaji,nikimaanisha kuwa shetani alikuwa anaamini kuwa pindi adamu
na eva watapomsaliti mungu basi mungu atawaacha wapweke na kwa sababu ya mateso
na masumbuko ya dunia watu hawa watashindwa kusitahimili mateso hayo na kufa na
kuacha mali zote chini ya hima yake muovu shetani.
Imani ya shetani
ilikuwa kuu akiamini kuwa hata kama wataweza kuzaa na kuongezeka basi kizazi
watachokizaa watakirisisha dhambi kuu ya ubinafsi ambayo ni kitovu cha ubepari na
mwisho wa nyakati watauana wenyewe kwa wenyewe wakigombania malisho na chakula.
Eneo
la wazi
Safari za
wafanyabiashara ziliwezesha kugundulika kwa bara hili la kwa mataifa ya magharibi na asia kwa
ujumla wake.Bara letu lilionekana kuwa eno la wazi lisilo na miliki wenye nguvu
kwa kuwa kulikuwa na makabila waliokuwa wamejitenga sana kiumbali na huku
yakijishuhulisha nza shuhuli mbalimbali ikiwemo uvuvi,ufugaji na mengine kilimo
basi nchi za bara la ulaya waliamua kwa dhati kushambulia bara hili kila kona
na kujichumia mali zilizopo na pia walichukuwa watu wa bara hili na kwenda
kuwafanyisha kazi ngumu kwenye mashamba na viwandani. Hakuna kilichokuwa si
mali kwao, vyote walibeba si pembe za ndovu,watu ,madini wala bidhaa za
utamaduni.Ingawa maeneo mengine walipata vizuizi kutoka kwa makabila kadhaa yaliokuwa na vifaa
vya kivita na kundi kubwa la wapiganaji lakini kwao haikuwa shida kubwa maana
walikuwa wamesha jipanga sawa sawa kuvunja kizuizi chochote kile kitachokuwa kinajitokeza
na kuzuia mpango yao.huku wakitengeneza ramani ya kuonyesha sehemu zenye mali
ikiwemo madini na maeneo yanayofaa kwa kilimo walifanya kazii hii kwa uangalifu
mkubwa.
SOMA KITABU HIKI CHOTE HAPA SASA
SOMA KITABU HIKI CHOTE HAPA SASA
No comments:
Post a Comment