KALENDA YA KIFO FULL STORY..ISOME SASA

KALENDA YA KIFO


Nikikumbuka tulivyokuwa utotoni sikuwahi hata tegemea kuna siku naweza kuwa hapa nilipo..
Ilikuwa ngumu sana kupata hata   mulo mmoja wa siku tuliishi kifukara sana sikuwahi vanguo mpya hata iwe sikukuu..
Mama alituzaa watoto saba na baba hana pesa kushona viatu ndo ilikuwa kazi yake..
Shule niliacha nikiwa la nne na kutimukia mtaani kutafuta maishaili niweze kusaidia wadogo zangu na familia yetu..
Kwa kweli tuliteseka sana nakumbuka hata nikienda msalani ilikuwa ngumu kujisaidia maana chakula tulichokuwa tunakula kilitufanya tushide kujisaidia bila kulia ..maana haja ilitoka kwa shida sana tulikuwa tumekonda sana afya mgogoro na hakuna aliyekuwa penda mtaani zaidi ya kutuita machokora.
Nakumbuka nilishawahi  lawitiwa na vijana wa kihuni usiku nikiwa stand nikiuza machungwa niliachiwa na mama..walikuja vijana na kununua machungwa yote na baada ya hapo walisema nikafwate pesa ndipo huko walinifanyia vitendo vya ajabu na nililia sana nilishidwa kutembea na walikuja kuibeba na kunipeleka hospital na baada ya kulazwa kwa siku tano ndipo niliruhusiwa kutoka na iliporudi nyumban nilikututa ndogo wangu wa tatu anaumwa sana na baada ya siku tatu alifariki dunia …siku ya mazishi yake nililia sana na sikuweza amini kilichotokea.majirani wachache walihuzuria kwa kuwa tulikuwa mafukara sana hatukuweza hata kununua jeneza tulimfunga kwenye kanga na vitenge na kwenda kumzika mdogo wetu.
Baada ya msiba baba yetu alisafiri na aliporudi toka kwenye hiyo safari yake alituambia kuwa leo ni siku yetu ya mabadiliko..na mimi nilishangaa sana kumuona baba amevaa nguo za bei na atabasamu kubwa alitutoa out na kutununulia mavazi mapya na kisha tukaenda kula kwenye baa kubwa pale mtaani kwetu ..

Kila mtu aliyetuona hakuna aliyeamini kwa  kuwa sisi si watu wa kupendeza wala wa kula sehemu zuri za bei ya juu..lakini kwa mara ya kwanza baba alitoa pesa mfukoni kwake elfu 10 ,na kwa wakati huo elfu kumi ilitutosha wote kula na kunywa na kusaza..

Baada ya siku hiyo mambo yalibadilika kabisa kabisa kwenye familia yetu..tulianza kuishi tofaut kabisa tulianza kubadilika na kuwa familia tofauti tulianza kupawa tunakula mara mbili mpaka mara tatu kwa siku..na baba alibadilisha kazi na kuanza kuuza nguo na wateja walikuwa kibao kiasi cha baba kuniweka na mimi ili nimsaidie kuuza mitumba na kwa siku tuliweza kukusanya elfu hammsini..

Tuliweza kubadilisha nyumba na kupanga sehemu zuri zaidi.maisha yalizidi kubadilika na kila siku nilikuwa namshukuru mungu na kusema  kweli mungu umetenda miujiza na huku nikimlaaumu mungu kwa nini mdogo wangu amekufa wakati huu maisha yameanza kuwa mazuri..
Baba alibadilisha kazi na kuhamia kwenye maduka ya bidhaa za nyumbani na alifunga maduka 5 makubwa mjini dar es salaam na tulikuwa watu  wa kazi na tulifanikiwa sana na tuliweza kumilki gari saba za abiria na mbili za kutembelea..pesa ilikuwa karatasi isiyo na dhaman kwangu tena maana nilikuwa na pesa na nilikuwa na uwezo wa kutembea mkoa ninao taka na nchi za jirani ..
Baba alikuwa aniamin sana na kila mtu alijua.baada ya mwaka baadae wadogo zangu wawili walikufa kwa ajali wakitoka shuleni na ulikuwa msiba mkubwa..na watu maarufu walihuzurua pamoja na wafanya biashara wezetu wa kariakoo..ilikuwa hudhunui kubwa kwetu na nijikuta Napata gazi na kuzimia baada ya kuona majeneza ya wadogo zangu wawili yakiingia kwenye nyumba yetu ya ostabey..
Nilizimia baada ya masaa 6 na nilipozindika nilikuta wameshawazika tayari sikuweza kutoka nje ya nyumba yetu kwa mwezi mzima..baada ya kuona mambo yanazidi kuniendea kuombo ilibidi niende kanisani kusali na nilianza kusali na nilisali kwa nguvu na baba yangu alikuwa ananiambia kuwa dini ni za wazungu sisi washwahili hatuna dini nilikuwa nambishia na nilikuwa namshauri aungane na mimi kanisani maana siku za kula mwanadamu duniani zinahesabika kabisa..lakini baba alikataa alisema yeye alijenga kanisa sasa ni kazi kwetu kwenda kusali ..yeye amestaafu na amepewa na pension yake kabisaa.
Sikukata tamaaa niliendelea kushawishi baba awe anahuzuria  kwenye ibada lakini niligoga mwamba kabisa..

Siku zilizidi kwenda na ikabidi nioe na kuwa na familia yangu na kuacha na baba na mama yangu tukahamia kwetu kwenye nyumba ambayo baba alitupa kama zawadi  siku ya harusi yetu tulibahatika kupata mtoto mmoja na kwa bahati mbaya alikuwa anaumbwa umbwa sana mara magonjwa yasiyojulikana hali hii ilitunyima rah asana mimi na mke wangu na tuliziduisha maombez na kwa kiasi kikubwa kila tulipo kuwa tunaomba mtoto wetu alizidi kupata nafuu..
Siku mmoja niliamua kwenda kijiji kwa baba na bibi na nilipofika huko nilikuta mambo ya ajabu sana maana nyumba ya bibi yangu ilikuwa na hali mbaya sana ingawa makaburi ya ndugu zetu yalikuwa yametengenezwa vizuri na sikuweza kuuliza kwa nini lakini kwa hali ile sikuweza hata kulala ilimpatia bibi pesa na kuwasalimia ndugu wengine na kuondoka zangu ..
Niliporudi dar niliitwa na mama yangu mzazi na akaniuliza ulienda kufanya nini kwa bibi yako nikamwambia kumsalimia alilia sana mama yangu na kusema umenipoza wanangu ..
Nikawaza sana kauli ya mama yangu nimempoza kivip bila ila jibu sikupata…na aliposema umenipoza tu aliondoka zake na kwenda kujifungia chumbani kwakwe..
Nilirudi na kuendelea na maisha na mke wangu na kwa wakati wote huo tulikuwa tunafaya biashara ya kuuza vipodozi ..na wadogo zangu waliobakia walikuwa wakisaidiana na baba kwenye maduka yake ya kariakoo..
Baada ya mwezi mama yangu mzazi alikufa na alienda kuzikwa kwetu kwa bibi..na nilimkumbaka alivyosema nimempoza ..maana hakuweza kufika kwa bibi akiwa mzima ..alirudi maiti na kila aliyekuwa pale msibani alikuwa anaogopa kusaliamiana na baba yangu na sikujua kwa nNI?
Lakini baada ya msiba kuisha kikao cha familia kilikaa na kumkalisha baba na wakaaza kumuuliza mswali kwa kilugha..
Wazee wa ukoo walimuulizwa …


Mzee mmoja :Kwa nini?????unafanya hivyo
Baba:sina jinsi
Mzee wa pili::huna jinsi kivip??
Baba:akanyamza kimyaaaaaa
Wazee walizidi kumtoromea kwa zama zamu na mwisho baba aliamua kuondoka naliporudi dar alikuwa kama amechanganyikiwa hivi ..?
Alikuwa anagawa bia kama maji akiingia baa anawanunulia wateja wote bia mpaka stock ya bia bar iishe kabisa na baada ya bia zote kuisha baba anakojolea kaunta ya bar na viti  na kulipa bili yake na kwenda zake..
Tabia hii ilikuwa ya kila siku baba akauza na gar zake akafili maduka yote kwa kugawa pesa kwenye pombe na akimaliza anakojolea kaunta ya mareti waliyoshidwa kumaliza kunywa watejaa..
Baada ya mwezi baba uchizi ulizidi kukuwa kiasi cha kuwa analala chooi na na kuamishi kila kilicho chake huko…wadogo zangu walitesema sana hawakujua cha kufanya naniliamua kuwachukua na kukaa nao kwangu…
Cha kushangaza baada ya miezi miwili kupita baba alirudi hali yake ya kawaida na alikuwa na pesa ajabu kiasi cha kujenga magorofa matatu kwa mkupuo ,maduka tisa alyafugua kwa mkupuo na alinunua magar matano ya kwenda mikoani ..
Sikuweza amini macho yangu baba huyu huyu chizi chizi juzi tu leo kafumuka hivi…ndipo nikaaza kutilia mshaka mali ya baba yangu na kuamua kupeleleza..
Siku ya kwaza iliianza upelelezi wangu kwenye maduka yake kwa ungalifu nilienda kama kusalimia tu..

Lakini baada nikagundua kila duka la mzee lina vitu vyote vipya kasoro saduku la kutumzia pesa t undo kuuukuu balaa na ni la ngozi…
Mfanyakazi mmoja aliniuliza sawali>>>?
Mfanyakazi:hivi kaka pale kwenu mnawafanyakaz wandani wengi sana eeeeee??
Mimi:hapanaaaaa kwa nini??
mfanyakazi:baba alisema hatuna haja ya kufagia duka wafanyakazi wa nyumbani huwa wanakuja kufagiaaaa
Mimi (kwa haraka):kweli…..
Baba aliporudi cha kushagaza alimfukuza mfayakazi Yule pale pale nikiwa naangalia .na hakuwepo na hakuna aliyewambia nilichaambiwa lakini alipofika akimfukuza kazi Yule mfayazi na mimi kuiuliza wewe mwanangu unafanya nin hapa??
Mimi:nimekuja kusalimiaaaaa
Baba:oooh kusalimia mkewo mzimaaa
Mimi:mzima kabisaaaa
Baba:wasalimie na ukija tena hapa uwe unato taarifa ili uikute siku hizi sishind sehemu mmojaa..
Mimi:sawa babaaaa
Nilipotoka pale ilienda yumbani kwa baba a nilipekuwa kila chumba kilichokuwa wazi na kufanikiwa kuona picha za marehemu wadogo zangu mama zikiwa  kwenye kalenda moja nyeusi na zilipangana kulingana na waliotangulia kufaa..katika mtiririko huo niliona picha yangu ikiwa ifwata baada ya mama nay a mtoto wangu ilinifwata mimi na mke wangu kisha wadogo zangu waliobakia na wamwisho alikuwa baba..
Ilishangaa sana na sikujuua ile kalenda ilikuwa ni ya nani ?maana chumba aliyokuwepo hiyo kalenda alikuwa halali mtu kabisa..
Ilirudi kwangu kwa hudhumi na kwambia mke wangu tusali sana maaana nyakati za mwisho zinakaribiaa na kweli tulizidisha maombi na kwa nguvu ya mungu tuliweza kuipinga roho ya kifoo…
Nilirudi tena kuingalia ile kalenda na kukuta picha yangu na familia yagu ni za mwisho kabla ya baba..picha za wadogo zangu zilitangulia baada ya mwezi mdogo wangu ambeye picha yake ilitangulia aliaza kuumwa sana ..


Mimi nikapata na kiwewe nikahamia nyumbani kwa baba yangu na familia yangu tukaaza kupiga maombi mazito kukemea ile kalenda ya kifo tulikemea na kwa kipidi chote hicho baba alikuwa hataki hkuja nyumbani kwake akisingzia nyumba yake tumeigeuzaa sinagogi..
Tulizidi kuomba na kumuombea mgojwaaa..na familia zimaa..siku moja iliamka asubuhi sana na kutazama nje nikawaona wadogo zangu pamoja na mama wakifanya usafi nje ya nyumba yetu ..
Nilipiga kelele kuu na kila mtu aliamka lakini walipokuja kuangalia hakuona kitu kwa kuwa mama na wadogo zangu waliokishwa kufa walikuwa tayari wameshapotea..
Ilichukua nyundo na kuanza kuvunja kila chumba  kilichokuwa kimefungwa bila kufumguliwa kwa muda mrefu ili kujua dsani kuna nini??
Wakati na anza kuvuja baba alipiga simu akanimbia umechokoza moto wanangu ..hii vita huwez kushinda nakujaaa.
Mimi sikuogopa cha baba wala msukule nilivunja chumba cha kwaza nikakutaa wafanyakazi watano wa
Baba waliokuwa wamekufa miaka ya nyuma wakiwa wamejikunyata kwenye kona,niliogopa kidogo na niliendelea kuvunja chumba 2 na sasa huko niwakuta wado go zangu wakila pumba na walikuwa na nywele za kichwani nyingi sana..niliia sana na kwa uchungu ilikuta naenda kuwakumbatia wadogo zangu kuaanzia ndogo wangu aliyekufa wa kwaza kipindi kile tulipokuwa na maisha magumu sana..




No comments:

Post a Comment