KALENDA YA KIFO
Nikikumbuka tulivyokuwa utotoni sikuwahi hata tegemea kuna
siku naweza kuwa hapa nilipo..
Ilikuwa ngumu sana kupata hata mulo mmoja wa siku tuliishi kifukara sana
sikuwahi vanguo mpya hata iwe sikukuu..
Mama alituzaa watoto saba na baba hana pesa kushona viatu
ndo ilikuwa kazi yake..
Shule niliacha nikiwa la nne na kutimukia mtaani kutafuta
maishaili niweze kusaidia wadogo zangu na familia yetu..
Kwa kweli tuliteseka sana nakumbuka hata nikienda msalani
ilikuwa ngumu kujisaidia maana chakula tulichokuwa tunakula kilitufanya tushide
kujisaidia bila kulia ..maana haja ilitoka kwa shida sana tulikuwa tumekonda
sana afya mgogoro na hakuna aliyekuwa penda mtaani zaidi ya kutuita machokora.
Nakumbuka nilishawahi
lawitiwa na vijana wa kihuni usiku nikiwa stand nikiuza machungwa
niliachiwa na mama..walikuja vijana na kununua machungwa yote na baada ya hapo
walisema nikafwate pesa ndipo huko walinifanyia vitendo vya ajabu na nililia
sana nilishidwa kutembea na walikuja kuibeba na kunipeleka hospital na baada ya
kulazwa kwa siku tano ndipo niliruhusiwa kutoka na iliporudi nyumban nilikututa
ndogo wangu wa tatu anaumwa sana na baada ya siku tatu alifariki dunia …siku ya
mazishi yake nililia sana na sikuweza amini kilichotokea.majirani wachache
walihuzuria kwa kuwa tulikuwa mafukara sana hatukuweza hata kununua jeneza
tulimfunga kwenye kanga na vitenge na kwenda kumzika mdogo wetu.
Baada ya msiba baba yetu alisafiri na aliporudi toka kwenye
hiyo safari yake alituambia kuwa leo ni siku yetu ya mabadiliko..na mimi
nilishangaa sana kumuona baba amevaa nguo za bei na atabasamu kubwa alitutoa
out na kutununulia mavazi mapya na kisha tukaenda kula kwenye baa kubwa pale
mtaani kwetu ..
Kila mtu aliyetuona hakuna aliyeamini kwa kuwa sisi si watu wa kupendeza wala wa kula
sehemu zuri za bei ya juu..lakini kwa mara ya kwanza baba alitoa pesa mfukoni
kwake elfu 10 ,na kwa wakati huo elfu kumi ilitutosha wote kula na kunywa na
kusaza..
Baada ya siku hiyo mambo yalibadilika kabisa kabisa kwenye
familia yetu..tulianza kuishi tofaut kabisa tulianza kubadilika na kuwa familia
tofauti tulianza kupawa tunakula mara mbili mpaka mara tatu kwa siku..na baba
alibadilisha kazi na kuanza kuuza nguo na wateja walikuwa kibao kiasi cha baba
kuniweka na mimi ili nimsaidie kuuza mitumba na kwa siku tuliweza kukusanya
elfu hammsini..
Tuliweza kubadilisha nyumba na kupanga sehemu zuri
zaidi.maisha yalizidi kubadilika na kila siku nilikuwa namshukuru mungu na
kusema kweli mungu umetenda miujiza na
huku nikimlaaumu mungu kwa nini mdogo wangu amekufa wakati huu maisha yameanza
kuwa mazuri..
Baba alibadilisha kazi na kuhamia kwenye maduka ya bidhaa za
nyumbani na alifunga maduka 5 makubwa mjini dar es salaam na tulikuwa watu wa kazi na tulifanikiwa sana na tuliweza
kumilki gari saba za abiria na mbili za kutembelea..pesa ilikuwa karatasi isiyo
na dhaman kwangu tena maana nilikuwa na pesa na nilikuwa na uwezo wa kutembea
mkoa ninao taka na nchi za jirani ..
Baba alikuwa aniamin sana na kila mtu alijua.baada ya mwaka
baadae wadogo zangu wawili walikufa kwa ajali wakitoka shuleni na ulikuwa msiba
mkubwa..na watu maarufu walihuzurua pamoja na wafanya biashara wezetu wa
kariakoo..ilikuwa hudhunui kubwa kwetu na nijikuta Napata gazi na kuzimia baada
ya kuona majeneza ya wadogo zangu wawili yakiingia kwenye nyumba yetu ya
ostabey..
Nilizimia baada ya masaa 6 na nilipozindika nilikuta
wameshawazika tayari sikuweza kutoka nje ya nyumba yetu kwa mwezi mzima..baada
ya kuona mambo yanazidi kuniendea kuombo ilibidi niende kanisani kusali na
nilianza kusali na nilisali kwa nguvu na baba yangu alikuwa ananiambia kuwa
dini ni za wazungu sisi washwahili hatuna dini nilikuwa nambishia na nilikuwa
namshauri aungane na mimi kanisani maana siku za kula mwanadamu duniani
zinahesabika kabisa..lakini baba alikataa alisema yeye alijenga kanisa sasa ni
kazi kwetu kwenda kusali ..yeye amestaafu na amepewa na pension yake kabisaa.
Sikukata tamaaa niliendelea kushawishi baba awe
anahuzuria kwenye ibada lakini niligoga
mwamba kabisa..
Siku zilizidi kwenda na ikabidi nioe na kuwa na familia
yangu na kuacha na baba na mama yangu tukahamia kwetu kwenye nyumba ambayo baba
alitupa kama zawadi siku ya harusi yetu
tulibahatika kupata mtoto mmoja na kwa bahati mbaya alikuwa anaumbwa umbwa sana
mara magonjwa yasiyojulikana hali hii ilitunyima rah asana mimi na mke wangu na
tuliziduisha maombez na kwa kiasi kikubwa kila tulipo kuwa tunaomba mtoto wetu
alizidi kupata nafuu..
Siku mmoja niliamua kwenda kijiji kwa baba na bibi na
nilipofika huko nilikuta mambo ya ajabu sana maana nyumba ya bibi yangu ilikuwa
na hali mbaya sana ingawa makaburi ya ndugu zetu yalikuwa yametengenezwa vizuri
na sikuweza kuuliza kwa nini lakini kwa hali ile sikuweza hata kulala ilimpatia
bibi pesa na kuwasalimia ndugu wengine na kuondoka zangu ..
Niliporudi dar niliitwa na mama yangu mzazi na akaniuliza
ulienda kufanya nini kwa bibi yako nikamwambia kumsalimia alilia sana mama
yangu na kusema umenipoza wanangu ..
Nikawaza sana kauli ya mama yangu nimempoza kivip bila ila
jibu sikupata…na aliposema umenipoza tu aliondoka zake na kwenda kujifungia
chumbani kwakwe..
Nilirudi na kuendelea na maisha na mke wangu na kwa wakati
wote huo tulikuwa tunafaya biashara ya kuuza vipodozi ..na wadogo zangu
waliobakia walikuwa wakisaidiana na baba kwenye maduka yake ya kariakoo..
Baada ya mwezi mama yangu mzazi alikufa na alienda kuzikwa
kwetu kwa bibi..na nilimkumbaka alivyosema nimempoza ..maana hakuweza kufika
kwa bibi akiwa mzima ..alirudi maiti na kila aliyekuwa pale msibani alikuwa
anaogopa kusaliamiana na baba yangu na sikujua kwa nNI?
Lakini baada ya msiba kuisha kikao cha familia kilikaa na
kumkalisha baba na wakaaza kumuuliza mswali kwa kilugha..
Wazee wa ukoo walimuulizwa …
Mzee mmoja :Kwa nini?????unafanya hivyo
Baba:sina jinsi
Mzee wa pili::huna jinsi kivip??
Baba:akanyamza kimyaaaaaa
Wazee walizidi kumtoromea kwa zama zamu na mwisho baba
aliamua kuondoka naliporudi dar alikuwa kama amechanganyikiwa hivi ..?
Alikuwa anagawa bia kama maji akiingia baa anawanunulia
wateja wote bia mpaka stock ya bia bar iishe kabisa na baada ya bia zote kuisha
baba anakojolea kaunta ya bar na viti na
kulipa bili yake na kwenda zake..
Tabia hii ilikuwa ya kila siku baba akauza na gar zake
akafili maduka yote kwa kugawa pesa kwenye pombe na akimaliza anakojolea kaunta
ya mareti waliyoshidwa kumaliza kunywa watejaa..
Baada ya mwezi baba uchizi ulizidi kukuwa kiasi cha kuwa
analala chooi na na kuamishi kila kilicho chake huko…wadogo zangu walitesema
sana hawakujua cha kufanya naniliamua kuwachukua na kukaa nao kwangu…
Cha kushangaza baada ya miezi miwili kupita baba alirudi
hali yake ya kawaida na alikuwa na pesa ajabu kiasi cha kujenga magorofa matatu
kwa mkupuo ,maduka tisa alyafugua kwa mkupuo na alinunua magar matano ya kwenda
mikoani ..
Sikuweza amini macho yangu baba huyu huyu chizi chizi juzi
tu leo kafumuka hivi…ndipo nikaaza kutilia mshaka mali ya baba yangu na kuamua
kupeleleza..
Siku ya kwaza iliianza upelelezi wangu kwenye maduka yake
kwa ungalifu nilienda kama kusalimia tu..
Lakini baada nikagundua kila duka la mzee lina vitu vyote
vipya kasoro saduku la kutumzia pesa t undo kuuukuu balaa na ni la ngozi…
Mfanyakazi mmoja aliniuliza sawali>>>?
Mfanyakazi:hivi kaka pale kwenu mnawafanyakaz wandani wengi
sana eeeeee??
Mimi:hapanaaaaa kwa nini??
mfanyakazi:baba alisema hatuna haja ya kufagia duka wafanyakazi wa nyumbani huwa wanakuja kufagiaaaa
mfanyakazi:baba alisema hatuna haja ya kufagia duka wafanyakazi wa nyumbani huwa wanakuja kufagiaaaa
Baba aliporudi cha kushagaza alimfukuza mfayakazi Yule pale
pale nikiwa naangalia .na hakuwepo na hakuna aliyewambia nilichaambiwa lakini
alipofika akimfukuza kazi Yule mfayazi na mimi kuiuliza wewe mwanangu unafanya
nin hapa??
Mimi:nimekuja kusalimiaaaaa
Baba:oooh kusalimia mkewo mzimaaa
Mimi:mzima kabisaaaa
Baba:wasalimie na ukija tena hapa uwe unato taarifa ili
uikute siku hizi sishind sehemu mmojaa..
Mimi:sawa babaaaa
Nilipotoka pale ilienda yumbani kwa baba a nilipekuwa kila
chumba kilichokuwa wazi na kufanikiwa kuona picha za marehemu wadogo zangu mama
zikiwa kwenye kalenda moja nyeusi na
zilipangana kulingana na waliotangulia kufaa..katika mtiririko huo niliona
picha yangu ikiwa ifwata baada ya mama nay a mtoto wangu ilinifwata mimi na mke
wangu kisha wadogo zangu waliobakia na wamwisho alikuwa baba..
No comments:
Post a Comment