SAFARI YA KUZIMU
Ilikuwa siku ya kawaida kwangu nilitoka kazini na kwenda
zangu nyumbani nikajumuikana familia yagu kama kawaida na usiku ulipofika
nililala na nilipo lala tu ndipo picha lilianza nilijikuta nimechukuliwa na
watu wasio julikana waliojifunika mashuka meusi na walikuwa wamebeba mapanga
yenye damu waliniweka juu ya fisi na gafla fisi tulitokea kwenye pori moja
kubwa na kulikuwa na watu wengi wakiwemo watoto wa dogo ,watu wazima na vijana …walikuwa
wanaimba nyimbo zisizoeleweka na walikuwa wakipiga makofi .nikiwa na naogopa
sana mmoja ya wale wachawi aliniambia karibu kwetu …
Unaona wale ni wezako tuliwachukua na kuwaweka msukule huku
ili wasaidi kazi kwenye nyumba zetu na maduka yetu..ndo maana maduka yetu
hatuweki walizi kabisa na wala hatuhitaji wafanyakaz wengi kwa kuwa hawa wote
wanatusaidia..kwa mfano angalia duka la mzee …. Unaliona akaionyesha kwenye
kioo na niliona vijana wengi wakiendelea na kazi usiku ule wakipanga vitu na
wengine wakifangia na kudek vibaraza…
Mchawi Yule alizidi kunionyesha naajabu ya kule kuzimu
alinipeleka stor yao huko nilikuta mafuvu ya vichwa na madumu mwengi ya
nanilipomuuliza yale madumu ni ya nini?aliiambia hayo yote ni store ya damu za
watu tunazozonyonya huko duniani ili kulisha vichanga vyetu vya huku..tuna
stock ya kutosha na kweli ilijaribu kuhesabu madumu lakin nilishindwa ..stor
ilikuwa kubwa kweli sijawahi pata kuona stor kubwa kama ile..tulienda upande wa
pili wa stor huku tulikuta nywele nyingi sana kiasi cha tan 700000 zikiwa
zimefungwa kweye marobota kama ya pamba
na nywele zote hizo zinatoka huku na
aliniambia wanazitumia kutengeneza magodoro ya kuzimu..
Tuliendelea kuikagua stor tulikuta mifupa ya watu na mengine
ikiwa na damu ana ile ya damu aliniambia ndo imetoka dunia muda si mrefu kwa
kuwa kuna ajali imetokea huko na moja ya wachawi alikuwa ni zamu yake kuleta
mifupa ndo maana inadamu kaileta hapa muda si mrefu..
Mbele kdogo nilikuta ngoz za watu zkiwa zimehifaziwa na
viungo baadhi ya watu kama vile macho,vidole na masikio..na vyote hivyo
hutumika na wachawi wanapoenda kuwanga wanavivaa na kuowaona wanafanana na mtu Fulani
kumbe si wao bali ni ngozi za watu waliochumwa wanazivaa ili kuficha usilia..
Tulitoka kweye stor na kupanda pembe ya mbuz na waliniambia
ifunge macho na nilipofunga tu nilitoke sehemu nyingine wao wanaita mahakamani
huko ndiko wanatoa huku nani afe na nani asife huku duniani hapo nilikutana na
wazee wenye nywele nyingi na wote hao walikuwa na mshale mkononi na mbele yao
kulikuwa na viyoo na picha za watu
zilikuwa zinatoke pale na jaji anaamua nani wamchome mshale ili afe ajee kuzimu
na kwa kuwa jaji alikuwa mkuu wa wachawi akichagua hata ndugu yako huwezi
kubisha ndivyo alivyoniambia Yule mchawi aliyekuwa ananitembezaa
Basi baada ya kutoka mahakani nilipelekwa kwenye chumba cha upasuaji na utoaji mimba huku ndiko
nilikuta na wadada wa kutosha na order za kutosha za kutoa mimba mwenyeji wangu
aliniambia huko duniani kuna watu wanataka mimba za wezao zitoke a sisi huku
tunafanya wanachokitaka na tunazitoa na kuzila ….na pia wale wanaofanyiwa
upasuaji sisi tunawaibia viungo vyao na wakauta wakufaa wakati wa upasuaji …wasiozaa
wote huwa tunawafunga vizazi hapaniliogopa sana maana chumba chote kilikuwa
kimetawaliwa na maiti za watoto na damu…
Baada ya kutoka hapo
tulielekea kweye chumba maalumu cha wasanii huku tulikutana na wasanii
maarufu wa dunia na nyimbo zao zinazotamba sana huko tulikutana na waimbishaji
na watungaji nyimbo ambazo waamini zikiimbwa dunia zitakuwa zinamtukuza shetan
na zitapendwa na umati wa watu..wasanii matajiri sana dunia niliwaona huko na
wote walikuwa wako bize wakifanya mazoezi na hizo nyimbo ili waje wazirokod
kwenye studio za huku na kuzirudisha kule zinabarikiwa na zinachinjiwa mtu
mmoja ili kutambikia na zinapotoka kila mtu lazima akubali ujio mpya wa msanii
husika..mwenyeji wangu alinielezea yote hayo..
Tulitoka huko na kwenda sehemu ya jikoni jiko la kuzimu ni
balaa tulikuta wapishi wengi na wengi walikuwa wakikaanga viungo vya watu na
kutengeza supu za damu za watu.gari la machinjio lilkuwa limejaa miili ya watu
wa kila rangi wanene kwa wembamba na wote walikuwa tayari kwenda kupikwa ili
baada ya ibada wachawi wote wanakuja kula na kunywa supu za wanadamu niliogopa
sana mwenyeji wangu akasema kila anayekufa huwa tunamfukua na kumla..tukishindwa
tunakojolea kaburi lake kwa hasira..ila wengi wa watu hawapo makaburini
wakizikwa sisi tunawala na tunakia migombaaaa..
Nilitolewa
pale maana kulikuwa kunameanza kukucha akaniambia nisimwambie mtu nilivyoviona huku antanichukua tena kesho usiku nije anitembeze maneno yaliyobaki kule kuzimu..
pale maana kulikuwa kunameanza kukucha akaniambia nisimwambie mtu nilivyoviona huku antanichukua tena kesho usiku nije anitembeze maneno yaliyobaki kule kuzimu..
Basi baada ya kufumba macho nilishituka nipo chumbani kwangu
kitandani na mwili mzima ulikuwa umejaa jasho na niliogopa sana na sikumwambia
mtu na nilitulia tuli..na niliendelea na ratiba zangu kama kawaida na ilipofika
mida ya usiku nilikwenda kulala na nilisali na kulala cha kushangaza ilijikuta
nimeamkaa asubuhi na yule mchawi hakuja kunichukuaaa..
Basi nilijitahidi kwa siku tatu nilikisali kabla ya kulala
na sikuweza kuchukuliwa kimuigiza lakini baada ya wiki nilizarau kusali
nikahisi yule mchawi kasahau kuja kunichukua kumbe nilikuwa najipozaaa mweyewe
siku hiyo alikuja na kunichukua na na
viboko juu nilipigwa kweli fimbo ..na ndipo nilipelekwa kweye ibada za kichawi
na huko nilikuta maajabu makubwaa sana..
Walikuwa wachawi wengi sana na wengi walikuwa wametoka
mtaaani kwetu na wengine ni wazugu kuna wachina na wahindi kila rangi walikuwa
wamekalia watu ..nikauliza hao watu ni wakina nani akasema hao watu ni wale
watu wa duniani wasio Sali wakilala huwa tunawachukua na kuwafanya makochi na
hasaa wale wanene ndio wafaa sana kukalia wanakuwa kama sofa vile..na wale
wembamba tunawatumia kama wahudumu wetu wa kuwatuma tuma tukiwa ibadani ..kila
mtu lazima awe uchi na lazima kila mwenye mke akae peke yake hakuna mtu na
mkewe kukaa sehemu moja…..
Mchawi
akazidi kunieleza::Tunasali kwa kuita mizimu na mizimu inakuja na kutukagua na
mizimu ina tupa maagizo toka kwa lusifa,,bosi wetu na tunapandishwa vyeo kulingana
na uwezo wa uuwaji wako kama unauwa sana na vyeo vinapanda sana ..mzimu mdiyo
inapokea wageni na wageni wote wanakabiziwa jini na wanatakiwa kwenda kulituza
dunia na nilazima lituzwe kulingana na mashati ya mizimu yetu ..hiyo tunawapa
wageni wetu na wengi hupewa majini ambayo yakionekana na watu wengine yaonekana
kama nyoka .
No comments:
Post a Comment