familia ya mazuzu (familia ya zero) sehemu ya 1

simulizi la kweli
familia ya mazuzu (familia ya zero)
sehemu ya kwanza..
0713592224
 jipe raha..
www.simulizizakweli.blogspot.com


ZERO FAMILY A.K.A MAZUZU FAMILY
Simulizi ya kuchekesha na kuelimisha ya familia yam zee zero,mama zero na mtoto wao mmoja zero wanaoishi ubungo dare s salaam…
Vituko vitu,familia hii ni majanga hakika….

Sehemu ya kwanza
Baba zero naondoka nyumbani na kwenda zake kwenye shuhuli zake za kila siku za kulinda nyumba ya muhind maeneoya kariakoo,huku akiwa ametinga jezi yake ya rangi ya kijani na yeboyebo chini huku akiwa na kirungu chake kwenye begi ,alikuwa akitumia usafiri wa baskeli kufika kazi na kurudi nyumbani kila siku,,,siku hiyo alikuwa amechelewa sana kazi ndipo alipoamua kuenda kituo cha polisi cha ubungo terminal na kukabizi baskeli yake ili apande dala dala ..alipokuwa aneelekea polisi mzee zero aliwaza atawaambiaje polisi ili waweze kumuhifadhi baskeli yake mpaka  atakaporudi toka kazini..basi alipata wazo kuwa awaambie polis kuwa baskeli hiyo ameiokota maeneo ya ubungo sheli,(oilcom)..
Alipofika kituoni
Aliingia na kuwasalimia maasikari waliokuwepo dhamu ziku hiyo kisha akakabidhi baskeli na kuwaambia kuwa ameiokota pale ubungo oilcom,askari walishangaa sana na kutaka maelezo zaid na mzee zero akawaambia anachelewa kazini mwenye baskeli akija mtampa m nawahi zangu kazini..afande mmoja akalazimisha andike maelezo tatizo likawa hapo maana mzee zero mwenye hawezi hata kuandika…basi polisi walimruhusu aende zake kazi na wakamuahidi kuwa wenye nayo akija watampa..mzee zero akikimbia zake mpaka stend akapanda gari akeenda zake kazini…
Alipofika kazini muhindi alimtukana sana kwa kuwa alikuwa amechelewa kazini na mzee zero akajitetea kuwa aliokota baskeli na ikabidi aipeleke polisindio maana alichelewa..muhindi akasema kama ndo hiyo basi tende nikaseme mimi ndo wenye baskeli…mzee zero kakubali na wakaenda wote toka kariakoo mpaka  ubungo wakaongea na maaskari kuwa muhindi huyo ndo wenye baskeli na aliisahau alipokuwa anaenda zake msikitini uliopo hapo sheli,askari wakampa ile baskeli na kumshukuru mzee zero kwa kuwa alionyesha utu wa hali ya juu,..
Baada ya kutoka polisi
Muhindi alimuahid mzee zero kumuongezea mshahara kidogo kwa kuwa amefanikisha kumpatia baskel ya bure kabisa..mzee zero akashukuru bosi wake na kumwambia hiyo baskeli ilikuwa ya kwake mwenye aliipeleka polisi sehemu yenye usalama ili aweze kupanda daladala awahi kazini..
Muhindi alishangaa sana ujasiri wa mzee zero na ujinga wake,basi alichokifanya aliamua kumuuzia baskeli yake na kumwambia kuwa hato pata mshahara ya miezi mitatu,pesa yake yote ya miezi hiyo itakuwa ni

malipo ya baskeli hiyo….mzee zero akasema sawa….

Je mzee zero atakubali???
fwatilia sehemu ya pili>

No comments:

Post a Comment