DIGITAL (SEHEMU YA PILI) USIKOSE KUISOMA

DIGITAL
SEHEMU YA PILI
USIKOSE KUSOMA SIMULIZI HII
NI ZAID YA SIMULIZI.

kuhakikisha je anayezikwa ni yeye kweli aliyekuwa amepiga picha kwenye magazeti akiwa na mastaa wa dunia pamoja na wahapa hapa bongo..
Toto la matumizi kama wengi walivyomjua bila kujua aliazia wapi mpaka kuwa staa wengi walibaki kusema tu..toto zuri toto la matumizi amekufa daa…wakiwa zaidi ya watu 900 kila mtu na lake alikuwa anajiropokea tu pale msibani..wengine wakisubiria makande na wali wa msibani..
Kikundi cha vijana wakiwa mbali kidogo na nyumba ya wazazi wa emm walianza kuimba wakisema emm umeenda mama,vimini atavaa nani???emm umeenda mama vimini atavaa nani??emm umeenda mama mikogo atafanya nani??emm umeenda mama gazeti atanunua nani??
Mwimbo huu walianza kuimba vijana wachache baada ya muda waliongezeka na kuzi kuimba kwa uzuni wengi wao wakiwa wameshalewa tayari na pombe za kienyeji na viroba..

Baada ya kuzikwa emm ,mwenyekiti wa mtaa alikuwa a machache ya kusema alianza kwa kushukuru watu wote waliohudhuria msiba wa ndugu yao,mwanao emm, na kusema mungu atawalipa kwa kupoteza muda wao kumfariji mama emm kipindi cha kuumwa kwa emm mpaka sasa hatua ya kumpeleka emm kwenye nyumba yake ya milele.
Akaendelea  kusema mwenyekiti::jamani ndugu zangu vijana na watu wazima kila mtu wa kijiji hili anajua emm alikuwa vipi kabla na baada ya kwenda mjini ..najua wengi mlikuwa mnapenda na wengine milikuwa mnachukia mnapoona  taaarifa za emm zilizokuwa zinatokea katika magazeti mbali mbali ya hapa kwetu..cha kujifunza tu ndugu zangu maisha hayana shortikati na kama shortkati ipo basi mwisho wake ni huu mama emm kateseka sana kuuguza mwanae bila msaada wa hao mapedeshe alikuwa anawaona na mwanae kwenye magazeti mbali mbali ya mjini…

Huku akiendelea kuelezea wasanii wezake walikuwa bize kuchukua picha kwa kutumia simu za bei ghali.wanaume roho za simba nao walikuwa bize kutongoza wasanii waliokuwa wamekuja pale msimbani kitu ambacho kilimfanya mwenyekiti apunguze urefu wa husia wake kwa kuwa alishaona watu hawamsikilizi kabisa..
Baada ya kuzika kila mtu alitawanyika na wasanii wote walirudi mjini wakamuacha mama emm na ndugu zake na rafiki wa karibu wa emm wa mjini mama z,ambaye baki kukabizi mali za mwanae emm alizoziacha ikiwemo gari lake aina ya Toyota mark 2,simu 5,samani mbali mbali kwenye chumba chake cha mjini na vitu vingine vidogo vidogo ilikwemo masanduku 20 ya nguo na na matano ya viatu..





Chapter 2:
Ratiba ya leo imeitinga shoga yangu yaani na mapedejee wane lazima nionae nao leo sasa sijui nijipangaje du..
Nana:wewe emm wane utawezaje sasa usije ukafa huko huko shoga yangu nakuonea huruma..
Emm;nife kivip huzi nilikuwa nao sita nikaondoka na milioni 2 na nusu fasta huoni nilipo rudi tu hapa nilikimbilia zahanati kuchukua dawa zetu zile ..
Nana:kumbe…..
Emm:ndo hivyo mama sema daktari wangu kasema nipunguze kidogo idadi wangu..maana kwa wiki moja tu ilikuwa nimeshatembea na wanaume 12.

 BONYEZA HAPA KUSOMA FULL STORY




No comments:

Post a Comment